Tuesday, November 9, 2010

KIROMO HOTEL,WENYEJI FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2010

Bodi ya wakurugenzi ya Miss Tourism Tanzania Organisation,leo wameitagaza hoteli ya kitalii ya Kiromo,kuwa wenyeji wa fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2010,zitakazofanyika mwezi Disemba 2010.

Rais wa taasisi hiyo ya Miss Utalii tanzania,gideo chipungahelo,amesema kuwa uteuzi huo umkuja baada ya kamati ya ufundi ya Miss Utalii Tanzania,kutembelea na kukagua hoteli mbalimbali zilizoko mkoani Pwani na Dar Es Salaam na kuridhishwa na ubora na viwango vikubwa vya kimataifa vilivyo navyo hoteli hiyo vya kuweza kuwa wenyeji wa matukio makubwa ya kitaifa na la kimatifa.Hii ni pamoja na ubora wa vyomba,migahawa na kumbi za kufanyia shindano hilo.

Jumla ya warembo 60 kutoka mikoa yote,kanda zote na vyuo vikuu vyote nchini wataingia kambini katika hoteli hiyomwanzoni mwa Disemba 2010, kuanza kambi ya fainali hizo za Taifa,ambazo zinaelezwa kuwa ni tukio kubwa la kitalii na kitamaduni kuwahi kutokea nchini.

washindi katika fainali hizo watawakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia na ya kimatifa ya Miss United Nation 2011,Miss Globe 2011,Miss Tourism 2011,Miss University Africa 2011,Miss Tourism University world 2011 na Miss Heritage world 2011.

No comments:

Post a Comment